A Confession Of A Mad Philosopher - Dizasta vina Lyrics
By: Admin | Artist: D dizasta vina | Published: 2024-21-09T05:05:59:00+07:00Lirikku.ID - A Confession Of A Mad Philosopher - Dizasta vina Lyrics: Halo Lirikku.ID, Dalam konten ini, kami menyediakan chord gitar untuk lagu "A Confession Of A Mad Philosopher - Dizasta vina Lyrics" yang dinyanyikan oleh Toton D dizasta vina. Dengan chord yang disajikan, pemula atau penggemar musik dapat dengan mudah memainkan lagu ini dengan gitar mereka sendiri. Kami menyajikan chord dengan akurasi tinggi sehingga pemain dapat mengikuti alunan musiknya dengan baik. Juga, kami akan memberikan informasi tambahan mengenai lirik lagu dan mungkin beberapa tips untuk menyempurnakan permainan gitar. Konten ini cocok untuk penggemar musik yang ingin belajar lagu baru atau bagi mereka yang ingin menikmati kesenangan bermain musik dengan gitar. Silahkan disimak A Confession Of A Mad Philosopher - Dizasta vina Lyrics Berikut Dibawah ini untuk Selanjutnya.
maana ya uhuru huisha baada ya utambuzi
baada ya kutambua kwamba uhuru si maamuzi
maana kifungo na mipaka vinafanana
aliyekuambia kuna uhuru utaupata kakudanganya
ipo asili inayofanya mwili wako mashine
kufanya ugonjwa uwe jela alafu afya ni jela nyingine
mjamaa amemwaga damu tayari
awe huru ili akawe mtumwa kwa mabepari
chagua kufa ukiona waja hawalipi wema
kufa wokovu kilichokufa hakifi tena
kufa ni uhuru kamili tabu ni nini
haupo huru sasa uhuru wa kweli ni kaburini
unak*mbatia uhuru wa kuambiwa
wakati unaishi na haukuchagua kuzaliwa
uhuru hautafutwi msafiri pumzika kubali chai
hauwezi kuwa huru ungali hai
uhuru si halisi jamaa badili umbo
uhuru sio jibu hata usikariri fumbo
uhuru ni falsafa ya vitabu iliandikwa na mababu
tutaisoma na mwisho itabaki huko
anayehitaji uhuru aelewe
kuogopa kufa ni utumwa kwa maana kufa ndio uhuru wenyewe
hata uwe mfalme ambaye anatoa idhini
huwei kuwa huru uhuru wa kweli ni kaburini
freedom freedom
freedom freedom
freedom freedom
freedom freedom
ukik*mbatia mw*nga jua utaificha nuru
uhuru si kwa mwafrika k*mkimbiza mkabulu
kuutaka uhuru sana jamaa si dalili njema
kama upo hai na unahisi uko huru fikiri tena
cheo huleta nuru pahala nuru haifiki
na pesa ndio njia ya uhuru ukiimiliki
pesa na cheo upita kule hakuingiliki
alisema mlevi mmoja ambaye pombe tu imemdhibiti
mwathirika ambaye dawa za kulevya zimefunga
na anahisi yuko huru mara baada tu ya kuvuta
labda si kweli haupo huru ukijiongeza
maana ukishaujua uhuru tayari ushaupoteza
je utaniona chizi au mwivi
au pumbavu au mshenzi ninayeongea vituko
au utaamua ukae chini utafakari
kisha ukakubali ndoa ajira navyo pia vifungo
aliye huru ni nani nieleze mtoto anayeenda kwa viboko
au mlokole mtenda mema baada ya kutishiwa moto
au msomi elimu mpaka chuo kihakiki
i swera kama uhuru ndio huo siuafiki
anayehisi yuko huru pita mbele
piga kelele maana hata mungu wako hayuko huru
hawezi kubadili mipango hawezi k*muumba
mungu mwingine mkubwa kupita yeye
unaetafuta uhuru wa kweli utateseka
utapoteza damu utatoa machozi na utakesha
hauwezi kuupata maana hakuna ulipouweka
uhuru haupatikani kwa fedha
uhuru is priceless kwakuwa si bidhaa halisi
wenye chapaa walihakiki
utaniangusha sana ukishindwa kuamini
upo uhuru ila uhuru wa kweli ni kaburini
you’ve got no freedom
you’ve got no freedom
you’ve got no freedom
you’ve got no freedom
freedom freedom
freedom freedom
freedom freedom
freedom freedom
Saksikan Video A Confession Of A Mad Philosopher - Dizasta vina Lyrics Berikut ini..
Random Song Lyrics :
- ブーケガルニ (bouquet garni) - 煮ル果実 (nilfruits) lyrics
- rip sears [bonus] - flowrpot lyrics
- you won't look back - cameron smith lyrics
- вбий мене (kill me) - crashmaestro lyrics
- wegue wegue - pongo lyrics
- tere bin - vee sharma lyrics
- иди ты на - vcho lyrics
- if you must leave my life - al martino lyrics
- munnah - geechi lyrics
- cinderella undercover (demo) - oingo boingo lyrics